Tuesday, October 29, 2013

KILA JAMBO LIPO KWA MAKUSUDI MAALUMU, SIKU MTAJUA TU.

Habari za ujenzi wa dunia jamani,
       Vipo viyu ambavyo ukiangalia sana unaona kuna kila sababu ya sisi kama watanzania kuwa na macho ya zaidi ya haya tuliyo nayo...kuna mambo yanatokea ukiyatafakari kwa kina unaona kunastofahamu nyingi mno zinazo acha maswali mengi sana vichwani na mioyoni..
     Sina hakika kama tutafika vema safari yetu kama watawala hawatakuwa na ile hali ya kwenda na wakati uliopo na tunaposema wakati uliopo tunazungumzia MABADILIKO CHANYA

Wednesday, October 23, 2013

TIBA MUBADALA KURUHUSIWA KUTUMIKA KATIKA HOSPITALI ZA SERIKALI

Hallow;;
   Katika hali isiyo kuwa ya kawaida mheshimiwa waziri mwenye dhamana ya afya BWANA MWINYI.amewatangazia watanzania kwamba muda si mrefu tutaanza kushudia tiba mubadala katika hospitali zetu za serikali..
     Sio jambo baya ni jambo zuri tena zuri sana.ila kuna mambo kadha ambayo mimi najiuliza na ningependa pia wanajamii tuungane pamoja kuuliza haya maswali kwa ndugu waziri..
  1--Je hawa waganga wa jadi au tiba mbadala watakuwa chini ya idara ipi itakayo waasesi.

2---Vigezo vya hawa waganga itakuwa ni jambo la wazi au ni siri kama ilivyo kawaida.

3---Serikali haina majengo je hawa waganga watakaa katika majengo yapi?

4---Serikali imejiandaa vya  kutosha kuruhusu hili jambo?

5---Kuna waaguzi na watoa tiba ambao wamerithishwa hizo huduma na babu au bibi zao.je mh Mwinyi ameliona hilo kwa jicho la karibu.

6---Maabara za kupimia hizo dawa zao zimeandaliwa na pia bajeti mwaka huu wa fedha itaongezeka kwenye wizara husika?
        Ninayo imani kubwa kwamba China ni moja kati ya nchi kubwa kiuchumi duniani,yenye idadi kubwa ya watu na pia yenye watalaam mbali mbali waliobobea katika fani hizo.....tumeiga huko. je itatusaidia kwa haraka......tujipe muda wa kufikiri kwa umakini...

Wednesday, October 16, 2013

kilimo diyo kipaumbele cha kwanza duniani kwa nini tanzania tunalala

Karibuni sana wapendwa,,
   Kwanza kabisa napenda kuwapongeza watanzania wote, kwa moyo wao wa kuendelea kuipenda nchi yao.ni jambo adimu sana kuongea na viongozi wakubwa kama nyie kwa amani kiasi hiki.
,nimepewa nafasi hii ya kuongea na watanzani na wasio watanzania kwa sharti moja kubwa.,sharti lenyewe ni gumu kuliheshimu ila kwa sababu bila kuliheshimu hilo hamtanisikiliza ,basi nitaliheshimu hilo pia kwa mashariti yakulinda utu wangu.
.
       Kuna mambo mengi ambayo yanatakiwa kuwa hai ili uhai wa taifa letu uendelee kuwa hai..kuna kila aina ya jitihada za viongozi wetu,kuhakikisha taifa letu linajikomboa,ni jambo zuri na naunga mkono jitihada hizo..kuna baadhi ya raia wenzetu ambao hawana mapenzi mema na taifa letu,walikuwepo,wapo na wataendelea kuwepo.

      Pamoja na kwamba wataendelea kuwepo,lakini tunalazimika kufanya jambo jepesi lakini litakuwa gumu sana kwa ndugu zetu viongozi,lazima watuelewe katika hili.

       KILIMO KWANZA-katika taifa lolote duniani hakuna kipaumbele chochote ambacho kinakuwa cha kwanza zaidi ya CHAKULA,Elimu,Afya,Ulinzi,ni moja kati ya vitu mhimu sana katika taifa lolote,lakini havichukui haki ya kwanza ambayo ni ya chakula,kinachomaanisha maisha ya binadamu.

        Huwezi kufanya jambo lolote bila kula,na hakuna taifa imara na lenye maamuzi juu ya wanachi wake kama taifa hilo litashindwa kuwapa chakula bora na cha kutosha wananchi wake,hii siyo dhana tu, bali ni uhalisia wa mambo ambayo yamethibitishwa na mioyo yetu na shahidi wetu akiwa ni macho yako na yangu..

      Tanzania siyo kisiwa, pamoja na kuwa na ardhi kubwa yenye rutuba ya kutosha bado tuaacha raia wetu wapoteze uhai wao kutokana na tatizo la chakula.,ni jambo la aibu kwa vizazi vilivyopita na kwa vizazi vijavyo kuja kusoma jinsi ambavyo babu zao ambao ndiyo sisi wa leo eti tulikufa kwa njaa ndani ya nchi hii ya Tanzania.

     Sina masikio ya kusikia kisichosikika ila nilipewa macho nione kile kinachoonekana,viongozi wa tanzania ya leo chini ya rais wangu ndugu Jakaya,wamepoteza uhalisia wa taifa letu kwa sababu ambazo nyingi ni sababu binafsi ambazo hata sebuleni kwa wanao huwezi kueleza,lakini leo ndizo sababu wanazotuambia katika majukwa siasa na katika machapisho mbali mbali..

    Maziwa makubwa matatu,mito isiyokuwa na msimu pamoja na maziwa madogo madogo zaidi ya mainne,leo tanzania inapokea msaada wa chakula kutoka japani,hii ni aibu ambayo haitafutika kamwe katika uso wa dunia,maana wao wanafikiri chanya na wanaandika historia,hatutakwepa aibu hii.

     Kuna mikoa miwili tu ya tanzania ambayo nchi kama nchi ikiamua kuwekeza hapo katika kilimo ndani ya miaka mitano tutazungumza hadithi za pato kubwa la taifa kutokana na kilimo na siyo kutegemea utalii na madini kama ilivyo leo.MOROGORO NA RUKWA,AU KIGOMA NA MBEYA,IRINGA NA RUVUMA,inanipa wasi wasi kwamba labda elimu ambayo viongozi wetu wanayo inafaa katika mazingira ya ULAYA NA ASIA na wala siyo TANZANIA.

      Naacha kiporo,hapo mwanzo nilizungumzia sharti nililopewa na ili maada iende sawa.MUNGU WANGU NDIYO KIONGOZI WANGU HUNIONGOZA MUDA WOTE...NILIAMBIWA NISIWE MBAGUZI NA NIWAPENDE WATU WOTE,,,ILA NIWE MPOLE KIASI KATIKA KULINDA NA KUTETEA UTU WANGU......KILIMO NDIYO UTAJIRI WA KWANZA DUNIANI...maana kila anyeitwa binadamu anahitaji chakula .

Tuesday, October 15, 2013

KILA KITU NA MUDA WAKE. HATIMAYE YAMETIMIA

KATIKA PICHA YA PAMOJA VIONGOZI WALIOANDAMANA KATKA MAJADILIANO  KUHUSU KATIBA MPYA

Sunday, October 13, 2013

KIOO CHA KWELI CHA DUNIA, NDUGU NYERERE MPENDWA WETU 14 YRS OUT OF US

Hakuna sababu yoyote ambayo kiongozi wa leo wa dunia hii hasa afrika ambaye hawezi kutambua na kuona mchango wa hayati mwalimu nyerere.
 Mosi-lugha yetu ya kiswahili n i lugha ambayo inazungumzwa na mataifa mengi kwa sasa ni moja kati ya lugha kubwa afrika;;;;nyerere.
  Mbili-zaidi ya makabila 120 ambayo yalizungumza lugha zao na kuwa na tamaduni zao,wameheshimu umoja wa kitaifa.nyerere
   Tatu-tulipewa heshima yetu na pia mataifa makubwa yote waliijua tanzania kwa misimamo yake...nyerere
    Nne--Alijenga shule na hospitali za watanzania wote bila kujali rangi,itikadi wala vyeo vyao-nyerere
KILA KITU KITAPITA TUU ILA UKWELI ULIOSIMAMIWA NA MWANADAMU MWENYE UPENDO WA KWELI UTADUMU DAIMA......HONGERA MWALIMU

Saturday, October 12, 2013

HAWA JAMAA NI WATU MHIMU SANA KATIKA NCHI YETU YA TANZANIA,Lakini kuna mambo ambayo yanatuchanganya sana raia wa kawaida ,waziri mkuu unacheo kikubwa sana kimaamuzi katika nchi hii.,sasa basi kazi ya waziri mwenye dhamana na ujenzi ni ipi?kwa sababu bwana pombe amesema yake na bwana mtoto wa mkulima umesema yako.
      Mnatuchanganya ile mbaya kuweni kama watu wenye ushirikiano wa kimantiki kabisa katika maamuzi yenu.mnatoka chama kimoja ,selikali moja,mwenyekiti wenu mmoja mr jakaya,wote mnaingia kutunga sheria na pia mnakutana kuwekeana viapo vya siri juu ya kulinda taifa letu......HII HAIJAKAA SAWA NA PIA HAIJENGI CHAMA CHENU NA INATOA UHALALI WA KUENDELEA KUWA MAWAZIRI KATIKA SERIKALI HII...MAANA HAMELEWANI,,,,

Friday, October 11, 2013

SIKU YA MTOTO WA KIKE DUNIANI

Tanzania tuadhimisha hii siku tukiwa bado na tatizo kubwa la ukeketaji kwa watoto wa kike,hii ni changamoto kubwa sana kwa viongozi wetu na jamii kwa ujumla wake,
  Maana tatizo la ukeketaji ni jambo ambalo kwanza linamnyima mtu haki yake ya msingi ya kuzaliwa,pili ni jambo hatarishi maana kuna magonjwa hatarishi mengi ya kuambukiza,na pia limekuwa linawaletea madhala akina mama wakati wa uzazi.
   Maoni yangu,wale wote ambao bado wanadhani ukeketaji ni mila yao wanayoiheshimu wote wamepitwa na wakati pamoja na mila zao,mabinti kataa katakata kukeketwa ukiona uazidiwa au unamheshimu mzazi basi hilo likianza kujitokeza kimbilia ofisi ya serikali ya karibu au polisi karipoti;
  Si kila kitu ni kizuri kwa watu maarufu igeni vile vyenye tija kwenu na vinavyo tukuza utu wa mtoto wa kike....GOD BLESS U ALLLLLLL

Tuesday, October 8, 2013

IKULU YAAKANUSHA KUSAINIWA KWA MSWADA WA MABADILIKO YA KATIBA NA MH.RAIS

Habari,
           Ikulu imesema kwamba muswada wa mabadiliko ya katiba uliopitishwa na bunge dodoma kwa mbwembwe kubwa na wabunge wa ccm bado haujasainiwa na mh rais,
          Imefikia hatua ya kukanusha kutokana na taarifa mbali mbali ambazo zilionekana katika vyombo vya habari mbali mbali asubuhi ya tarehe 8 october 2013.
         Inakuwa kama sinema fulani ambayo inasubiliwa kwa hamu kubwa na watazamaji wake ambao ni watanzania kwa ujumla wake...hapa kuna makundi mawili ya watanzania ambayo kila kundi wanataka kuona sinema ya aina tofauti katika kitambaa kimoja tena kwa wakati mmoja,kuna kundi la wapenda mabadiliko chanya na kundi la wapenda mabadiliko hasi,

Hawa  wote wanavutana sana lakini mshindi siku zote ukweli huwa unashinda hata ukicheleweshwa kwa nguvu ya dola bado siku utakuja kushinda.MUNGU IBARIKI TANZANIA WAJALIE HEKIMA NA BUSARA VIONGOZI WETU ILI WALIONGOZE TAIFA VEMA NA WAFANYE MAAMUZI  YA HEKIMA

Sunday, October 6, 2013

NIMEAMBIWA,,KAULI YA RAIS ILIYOJIRUDIA SANA KATIKA HOTUBA YAKE,NINI HASA MANTIKI YAKE.

Salamu ndugu zangu mabibi na mabwana,habari ya jumapili tulivu,.-----Kwanza kabisa napenda kutoa shukrani zangu za dhati kabisa kwa rais kikwete,jopo la washauri na mama salma kwa kumshauri mheshimiwa na hatimaye kujaribu kukemea kile kinachoonekana kama ni tishio kwa amani ya taifa letu.
  Kwaninini nasema kile kinachoonekana kama ni hatari kwa taifa kumbe si hatari, bali ni uastawi wa demokrasia na utafutaji haki kwa amani kutoka kwa watawala,nimesikiliza kwa umakini sana hotuba ya rais wangu na nikaamua niirudie tena ili nisipitwe na japo neno moja.
   Katika hotuba ile kuna mambo mazuri mengi na yenye tija kwa taifa hili, Na yale ambayo watu walioamua kufikiri chanya walitaka kuyasikia basi tuliyasikia kwa asilimia kubwa japo yapo mengine muhimu hatukusikia, ila siku zote hatujachelewa tuanze pale tulipo
   Kitu mhimu leo ambacho nataka tujifunze watu wote hasa watu wa karibu na rais, watendaji na hata washauri.hili neno NIMEAMBIWA, je  neno hili lilikuja kwa bahati mbaya au lina ajenda ya siri ambayo hata wasaidizi wake hawaijui,watendaji na wasemaji wa chama dola na serikali hawaelewi mtego uliopo hapa wao wanadhani KATIBA ni kwajili ya uchaguzi wa 2015,lakini pamoja na kwamba ni mhimu kuwa na katiba bora 2015.mnasahau kwamba bila kufanya maamuzi yenye hekima na busara kwa masilahi ya taifa 2015 mtajibiwa ninyi kwenye sanduku la kura na raia hawa wa tanzania wenye umasikini wa kutupwa,
    BWANA Jakaya atakuwa anakula mafao yake na wastaafu wenzie  na kuendeleza miradi na asasi mbali mbali za kifamilia,je?Chikawe,Bulembo,Nape,Wasira,Lukuvi,Shigela,Ndugai,Mwigulu,Lusinde,pamoja na vyeti vyenu vingi,tena vyenye alama nzuri,mnachukua mambo mazito mepesi kiasi hicho?,basi kama lengo lenu ni kwenda likizo isiyo na malipo 2015 katika siasa kama Jakaya  na Bwana Pinda basi endeleeni na kutokusoma alama za nyakati ......ADUI YAKO NI YULE WA KARIBU YAKO,KILA JAMBO NA MAJIRA YAKE YATIMIAPO MAJIRA ANAYEWEZA KUBADILISHA MAJIRA HAYO NI MUNGU PEKEE.Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika



Friday, October 4, 2013

HII NDIYO HEKIMA YA MTU ANAYEITWA RAIS YANAPASWA KUWA;

Hongera sana mheshimiwa rais,unastahili pongezi kubwa katika hekima hiyo uliyoionesha kwa wananchi wa tanzania,hata wale waliokuwa na misimamo yao hasi,basi lazima tuwe na utayari wa kukubaliana katika mambo kadha wa kadha yahusuyo mstakabari wa nchi yetu......LIPUMBA,MBOWE,MBATIA,jitihada zenu ni kubwa na njia yenu imeonekana,

Thursday, October 3, 2013

PAMOJA NA MATESO YALIYOPO DUNIANI LAKINI BADO TUMAINI LETU NI YESU


Hata wakati ambao mambo yanakuwa ni magumu sana,kumbuka kwamba yupo bwana mtetezi wako ambaye alichukua magumu yako na mateso pale msalabani------
-KWA IMANI KUBWA BADO AFRIKA BARA LANGU TUNAZIDI KUMTAFUTA KWA NGUVU JAPO MAZINGIRA NI MAGUMU,,,FUTA MUNGU Mungu wetu anatuahidi kwamba yale tuliyoyakosa duniani tutayapata mbimbuni


MTOTO AKIWA KATIKA KIMBILIO LA KWELI AMBAYE NI MUMBA WA MBINGU NA NCHI-----

KUNA KILA SABABU YA WATANZANIA KUTUMIA HEKIMA ZAO NA BUSARA KATIKA MCHAKATO WA KATIBA

Kundra za mwenzi mungu zinahitajika,,,,
           Kwanza kabisa napenda kutumia nafasi hii kuwakumbusha watanzania kwamba kila kitu katika nchi yetu kipo ili watu waendelee kuishi,nashawishika kuamini kwamba bara zima la Afrika ni lazima tufanye mabadiliko makubwa sana katika sekta hii ya kisiasa.
  Siasa imekuwa mwiba wa uchungu sana kwa maendeleo ya wana wa afrika,kwa maana gani?kila nchi ya hapa Barani Afrika imepata matatizo ya yatokanayo na siasa, katika siku za za hivi karibuni nchi yangu ya tanzania imeingia katika mchakato wa kupata KATIBA MPYA YA NCHI.
      Ipo nia ya dhati kabisa kwa baadhi ya viongozi wa siasa na wapo pia ambao nia hiyo haionekani katika mioyo yao bali inaonekana katika macho yao.unapata wakati mugumu sana kuelewa,,Nani ni nani katika nchi hii,yupi anamaamuzi yapi,kauli ipi ndo kauli ya mwisho,maana sasaivi kila mtu anasema, tena maneno mazito ambayo ukiyatafakari sana, unaona kama angekuwa mtoto tungesema huyu mtoto amedekezwa na wazazi au walezi wake.,maana mheshimiwa RAIS ambaye ndiye amiri jeshi mkuu wa nchi hii yupo na yupo kimya,japo kimya kingi kinashindo mkubwa lakini kwa Afrika yangu bado ni kitendawili kikubwa ambacho labda huunda kikaja kuteguliwa na kizazi cha mabadiliko ambacho bado sijakiona kwa macho ya ndani ila katika macho ya nyama kizazi hiki kipo.
  Kuna muungano wa vyama vya siasa hapa na baadhi ya asasi ambazo zimetoka wazi wazi kupinga muswada uliopitishwa na BUNGE( JMT)pale dodoma.waliopitisha ni wabunge na wanayohaki  ya kufanya kile walichokifanya,hiyo itabaki kuwa hivyo.
  Hakuna hoja ambayo itakuwa hoja ya maana sana kuliko hoja nyingine,kama watu wachache wanaweza kuchukua haki ya mtu ya msingi ambayo amezaliwa nayo na kufanya hiyo haki imezwe na itikadi ya kundi fulani.kwa hiyo hapo hoja hiyo, itakuwa haina maana yoyote ile kwa mtu huyu.
  Jaji warioba na timu yako mmefanya ya kwenu,mazuri na yameonekana kwa macho,haya yote yanayotokea ni kutokana na uhalisia mliouweka katika rasimu hii ya kwanza ya katiba,endeleeni kuwa na hekima na siku ya kufanya maamuzi magumu basi fanyeni maamuzi yenye hekima na busara ili kumbu kumbu yenu ibaki katika vizazi na vizazi,,
  MH RAIS, Miaka kumi ya ikulu ni miaka mingi sana katika kuweka historia,  Histori kwa kawaida zipo za aina mbili tu,historia mbaya na historia nzuri ya kukumbukwa na kuigwa na vizazi. kwa umri wako mh rais kiongozi wako mkubwa na wa kwanza tena  mtetezi wako ni HEKIMA NA BUSARA maana hutoka kwa mungu.tazama kwa makini na uamue kwa makini maana amani  ya nchi hii ipo mikononi mwako..itikadi zetu zitapita ila nchi na ardhi ya tanzania itabaki daima.
     Kama kuna jambo raisi duniani basi ni kuwa na upendo kwa jamii inayokuzunguka ila ni nadra sana kwa watawala wa dunia hii kuona hilo,,,MUNGU IBARIKI TANZANIA ,WABARIKI VIONGOZI WAKE UWAPE HEKIMA YA MAAMUZI...

Wednesday, October 2, 2013

ISRAEL TAIFA LA MUNGU LENYE KUJIAMINI ;

Israel ,
 Jamaa hawak nyuma na kujilinda na kulinda mipaka ya taifa hilo ambalo limezungukwa na maadui pande zote.lakini kwa sababu israel ni taifa teule limekuwa na misuguano mingi na mataifa hayo jirani.
  Leo kuna kitu kimoja ambacho kimesaemwa katika vyombo vingi vya habari ,pale waziri mkuu wa Israel,alipoiambia dunia kwamba IRAN inatengeneza siraha za nyukiria na wako tayari  kama taifa la israel kuhakikisha mpango huo unakoma mara moja, hata kama umoja wa mataifa hautaunga mkono ila wao wako tayari kuona nyukiria haiendelei IRAN.
     Hapo hapo Rais wa IRAN Bwa, ROHANI anasema wao wataendelea kutengeneza kwajili ya usalama wao.HILI SIYO JAMBO LA MASIHARA KASISA KATIKA DUNI

A .tafuteni suruhuu viongozi wetu....
                                                                                                                                                                 

ULIVYO LEO NI MATOKEO YA MAWAZO NA MAAMUZI YAKO YA JANA

Hapana shaka katika hili ndugu zanguni,habari zenu za ujenzi wa dunia hii tuipitayo,.
Leo nataka tujue au tujufunze kitu kidogo tuu ila chenye maana kubwa sana katika maisha ya binadamu hapa duniani na maisha baada ya kifo.
 Vile ambavyo tunaishi leo ndiyo hivyo tunavyotengeneza maisha yetu ya kesho ama tukiwa hai au tukiwa katika hali ya namna nyingine si jinsi ya miili hii tuliyonayo.
  Katika maisha ya kawaida tunadhani kwamba sisi twajua kila kitu lakini kwa bahati nzuri mungu wetu ni yeye asiyechunguzika mwisho wa kufikiri kwetu mwanzo wa wake wa hekima,napenda sana kuawmbia ndugu zangu ukishindwa kutambua kwa kamilifu kwamba yapo maisha mengine baada ya kifo basi utapata shida sana hata kutambua baadaye yako.
  Maamuzi ya mtu ndiyo hupima kwamba ni kwa kiasi gani anafahamu asili yake na asili ya maisha ya mwanadamu hapa duniani.
  Ili kuwa na kesho yenye matumaini lazima umuishie kristo yesu, umkaribishe katika moyo wako na aishi ndani yako siku zote za maisha yako. kinyume na hapo utapotea ndio maana mwimbaji mmoja wa nyimbo za injili aliimba wimbo mmoja usemao PEKEE YANGU SIWEZI.
      Pekee yako huwezi kumshinda mfalme wa anga ibilisi shetani,ambaye kila sekunde ya pumzi yako  anataka uwe mufuasi wake ili shimo la moto liambatane nanyi wakati wa hukumu ya haki...
           MTETEZI WETU YUU HAI tutende  yale aliyoyaamuru bwana wetu yesu kristo ili tukavishwe taji zetu baada ya kazi tuliyotumwa duniani kutimiliza   BARIKIWENIJ